FAIDA YA LIMAO MDA WA ASUBUHI
FAIDA 6 ZA KUNYWA MAJI YA NDIMU / LIMAO KILA ASUBUHI
Unaambiwa kunywa maji kwa wingi hasa wakati wa asubuhi ni faida kubwa sana kiafya mwilini, lakini kunywa maji ya uvugu vugu yenye ndimu / limau ni faida mara dufu.
Hii ni kutokana na vitamin C iliyomo katika matunda haya ambayo ni faida kubwa sana katika mwili wa mwanadamu.
Mbali na vitamini C, ndimu ina vitamini B-complex, madini ya Kalshiamu, chuma, magnesiamu na potashiamu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa (apple) au Zabibu.
Kunywa maji peke yake ni ngumu kwa baadhi ya watu kutokana na kupata kichefuchefu lakini maji yaliyotiwa ndimu au limau huwa na ladha nzuri na kila mtu anaweza kunywa bila tatizo.
Hapa nimekuorodheshea faida 6 za kunywa maji yenye ndimu / limau kila asubuhi.
Tiba dhidi ya kikohozi
Tumia limau katika maji ya uvuguvugu, weka na asali kidogo. Mchanganyiko huu husaidia kutibu mafua na kikohozi.
Faida nyingine ni pamoja na;-
Kuondoa harufu mbaya mdomoni
Huboresha kinga ya mwili
Husaidia kusafirisha damu mwilini
Husaidia kupunguza uzito
Kinga dhidi ya saratani
Anza siku yako kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku
Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.
Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.
Comments
Post a Comment