KITUNGUU MAJI,TANGAWIZI MGANGA WA NYWELE ZILIZOKATIKA

 Nywele kuwa nyepesi na kukatika kwa nywele  ni tatizo sugu kwa baadhi ya watu haswa kwa wanawake. Watu wengi wanapoteza pesa nyingi wakihangaika huku na kule kutafuta suluhiso juu ya tatizo hili. Leo nataka nikujuze namna ya kupambana na tatito hili kwa kutumia tangawizi na kitunguu maji tuu.

Tangawi na  kitunguu saumu ni viungo tunavyovitumia jikoni kila siku katika upishi lakini viungo hivi tunaweza kuvitumia pia kwenye nywele kukabiliana na tatizo la nywele kuwa nyepesi.

Tangawizi imesheheni madini ya magnesium, potasium , phospate pamoja na vitamins ambavyo vinasaidia nywele kuwa zenye afya na hivyo kuzuia kukatika kwa nywele.

Kwa upande wa kitunguu maji kinasaidia kupambana na bacteria wanaoweza kusababisha magonywa ya ngozi ya kichwa kama m’ba ambayo huchangia kukatika kwa nywele.

Ili kutumia viungo hivi kama tiba kwa nywele zako unatakiwa kusaga tangawizi pamoja na kitunguu maji chako kisha kuvichuja na kupaka mchanganyiko huu kwenye ngozi ya kichwa chako, tumia kofia ya plastiki kufunika nywele zako kwa dakika 15 na baada ya hapo osha nywele zako kwa maji baridi na shampoo kidogo.

Kuna msemo unaosema “Ukitaka kupata mazao mazzuri basi andaa ardhi yako vizuri”, vivyo hivyo kwenye nywele ukitaka kuwa na nywele nzuri zenye afya una budi kuandaa ngozi yako ya kichwa vizuri.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA LOTION YA KUNG'ARISHA USO NA MWILI MZIMA

MAFUTA YA MNYONYO

FAIDA YA TANGAWIZI KATIKA MWILI.