JINSI YA KUTENGENEZA MAZIWA YA SOYA NYUMBANI

 UANDAAJI MAZIWA YA SOYA UKIWA NYUMBANI



Maziwa ya Soya

Aina hii ni maarufu pia, na kwa kuwa yanatokana na mimea, maziwa haya hana cholesterol ( lehemu) - tofauti na maziwa ya kawaida. Maziwa ya Soya pia yana kiwango cha chini cha kalori kuliko maziwa ya ng'ombe, yana kalori takribani 130 kwa kila kikombe. Hakuna lactose  katika maziwa haya, aina ya protini inayoleta sana gesi tumboni, hivyo huyafanya kuwa mbadala muhimu kwa watu ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa kushindwa kuvumilia lactose (lactose intolerance) katika mfumo wao wa umeng'enyaji, pamoja na watu wasiotumia bidhaa zitokanazo na wanyama pia (vegeterians) sababu haitoki kwa wanyama. 


Soya ni mboga nzuri sana, na maziwa yanayotokana na jamii hii yana utajiri wa potasiamu, protini na kalsiamu ikiwa mtengenezaji atayaimarisha na madini. Pia ni chanzo kikubwa cha vitamini A na vitamini B12, ambayo haipo katika aina nyingine za maziwa.

Maziwa ya Soya hutoa kiwango cha juu cha protini, pia ni bora kwa watu ambao wanajaribu kudhibiti uzito wao au kupunguza mafuta. Pia ina kiwango cha chini sana cha mafuta, ikilinganishwa na aina nyingine za maziwa. 


Moja ya masuala mabaya ya maziwa ya soya ni kwamba kunywa kwa wingi kunaweza kuwa na athari mbaya kwenye uzalishaji wako wa homoni, hivyo wale walio na matatizo ya tezi wanapaswa kuepuka kunywa maziwa haya, au kufanya hivyo tu na ruhusa ya daktari wao.


Jinsi ya kuandaa maziwa ya soya ukiwa nyumbani


Anza kwa kuichambua soya yako,  toa uchafu ioshe kisha iloweke kwenye maji kwa kipimo cha, vikombe viwili vya soya kwa maji lita moja, loweka soya yako kwa masaa 8.


Mwaga maji kisha toa maganda, hakikisha maganda yote yametoka. Maganda ya soya yana aina ya protini inayozuia aina zingine za protini kufyonzwa mwilini kama virutubisho hivyo tunayatoa kuepuka hili. Lakini si kwamba soya ina sumu kama ambavyo inafahamika na jamii kubwa.


Osha tena soya zako na maji safi


Anza kuweka kikombe kimoja cha soya kwenye blenda na maji safi na salama mililita 600 kisha saga hadi upate ulaini kaa juice au maziwa, rudia kusaga na soya zingine zilizobaki hivyo hivyo kwa kipimo hiko cha maji hadi soya zako ziishe.



Kisha mimina mchanganyiko wako kwenye sufuria safi na uchemshe mchaganyiko wako kwa moto wa kawaida hadi uchemke vizur, usikae mbali maana yanapanda juu kama maziwa ya ng'ombe, endelea kuchemsha kwa dakika angalau 20 huku ukikoroga.


Wakati unakoroga toa utando unaotokea juu kama ule wa maziwa ya ng'ombe tunza kwenye fridgr unaweza tumia kuungia mboga zako au chakula.


Zima jiko ukiona yameshachemka vizur, kisha chuja maziwa yako kwenye bakuli safi au jagi, tumoa chujio safi unaweza kuweka kitambaa kisafi cheupe juu ya chujio ili upate maziwa masafi zaidi


Unga unga utakaobaki unaweza pia kuutunza ukawa unaungia vyakula vyako, nao una virutubisho vingi hasa protini


Yaache maziwa yako yapoe kisha mimina kwenye kitunzio chako, labda ni chupa au glasi, unavyomimina unaweza tumia chujio pia ili kuhakikisha unapata maziwa masafi zaidi.


Maziwa yako yapo tayari kwa matumizi. Unaweza ukayanywa bila sukari au ukaweka sukari

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA LOTION YA KUNG'ARISHA USO NA MWILI MZIMA

MAFUTA YA MNYONYO

FAIDA YA TANGAWIZI KATIKA MWILI.