TIBA. KWA KUTUMIA TANGAWIZI
NAMNA YA KUTUMIA
TANGAWIZI KWA TIBA
NAMNA YA KUTUMIA TANGAWIZI
KWA TIBA
Kutibu kutokusagika kwa chakula
tumboni, Gesi tumboni, Msokoto
wa tumbo (bila kuharisha),
Kutapika, Mshtuko/Mkazo wa
ghafula (wa msuli),Maumivu ya
tumbo na Kibofu cha mkojo
ikiambatana na Homa, Mafua,
Kukohoa na Pumu.
TUMIA JAM YA TANGAWIZI.
JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA
TANGAWIZI.
Kamua TANGAWIZI mbichi kisha
changanya maji yake (Juice) na
Sukari. Chemsha mpaka
mchanganyiko huo uwe mzito.
Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki
iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa
na karafuu iliosagwa. Iweke dawa
hii vizuri na tumia inapo hitajika.
KWA KUVIMBIWA NA KUTAKA HAMU
YA KULA.
Changanya Juice ya TANGAWIZI,
Juice ya Limau na Chumvi Mawe
kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha
umechanganya vizuri. Kunywa dawa
hii kabla ya Chakula.
Vingineyo changanya vipimo vilivyo
sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI
na Sukari Mawe. Koroga vizuri,
kunywa kabla ya kula chakula.
Dawa hii husafisha Ulimi na Koo
na hukuongeza hamu ya kula na
kukufanya mchangamfu.
MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA
SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya
Tangawizi.
KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu
kwa Juice ya Tangawizi.
KWA KISUKARI
Kunywa Juice ya Tangawizi
iliyochanganywa na Sukari mawe.
KIUNGULIA, KUKOSA HAMU YA KULA
NA BAWASIRI
Tumia Samasarkara Churna.
KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya
Tangawizi na Juice ya Kitunguu.
MAUMIVU YA KICHWA CHA
WASIWASI
Changanya Juice ya Tangawizi na
Maziwa, kisha kausha. Nusa unga
huo kama Tumbaku.
MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au
viwili vya Tangawizi iliyosagwa na
kijiko kimoja au viwili vya mafuta
ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja
mara mbili kwa siku.
BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha
Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya
maji kunywa mchanganyiko huu
ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike
mpaka utoe jasho.
KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA
KICHWA
Chukua Tangawizi ya Unga koroga
na maji kidogo iwe nzito kama
tope. Jipake na uchue kwenye paji
lako la uso kabla ya kulala. Kwa
Jino jipake na uchuwe kwenye
Comments
Post a Comment